pmbet

"Someni kwa bidii muwa madaktari na wauguzi" - Dr. Janabi

Sisti Herman

September 16, 2024
Share :

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili umekutana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani kwa lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya afya, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanafunzi hao kusomea masomo ya sayansi ili kujiandaa kuwa madaktari na wauguzi wa baadaye.

Akizungumza na wanafunzi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi, amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao sambamba na hilo kutambua uwezo wao wa kufikia mafanikio makubwa katika taaluma za afya.

“Wanawake wana uwezo wa kufikia nafasi za juu katika jamii, kama tunavyomshuhudia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni mfano mzuri wa uongozi thabiti na hili linawezekana endapo mtajituma, kusoma kwa bidii, na kufuata malengo yenu kwa uthubutu,” amesema Prof. Janabi.

Ameongezea kuwa sekta ya afya inahitaji wataalam wengi zaidi, hususani katika kada za udaktari na uuguzi, kwa kuwa ni sekta nyeti inayohitaji nguvu kazi kubwa ili kuboresha huduma za afya kwa watanzania.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet