pmbet

Southampton matatani kwa kuchungulia mazoezi ya timu pinzani

Eric Buyanza

May 9, 2026
Share :

Klabu ya Southampton imeingia matatani baada ya kushtakiwa kwa kukiuka kanuni za EFL kwa kufanya ujasusi wa kurekodi mazoezi ya Middlesbrough.

 

Ligi ya Soka ya Uingereza ilipokea malalamiko kutoka kwa Middlesbrough juu ya madai ya kunaswa kwa mtu wa Southampton akirekodi mazoezi yao kabla ya mechi ya mkondo wa kwanza itakayofanyika Jumamosi ya leo kwenye Uwanja wa Riverside.
 

Tukio hilo linafufua kumbukumbu za tukio kama hilo wakati Ligi ilipoipiga faini ya pauni 200,000 klabu ya Leeds kwa kupeleleza mazoezi ya klabu ya Derby County kabla ya mechi kati ya vilabu hivyo viwili Januari 2019.
 

Taarifa ya EFL siku ya Ijumaa usiku ilisomeka: "Klabu ya Soka ya Southampton leo imeshtakiwa kwa ukiukaji wa Kanuni za EFL, na kesi hiyo itapelekwa kwa Tume Huru ya Nidhamu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet