Southgate ajiuzulu ukocha Uingereza
Sisti Herman
July 16, 2024
Share :
Baada ya kushindwa kutwaa taji la kombe la mataifa Ulaya (EURO 2024) kocha wa timu ya Taifa Uingereza Gareth Southgate amejiuzulu rasmi kufundisha timu hiyo aliyojiunga nayo mwaka 2016. Akiwa na Uingereza kocha huyo ameiongoza timu hiyo kwenye mechi 102, akishuhudia ushindi mara 61, sare 24 na kufugwa mara 17. Pia amefanikiwa kuifikisha hatua kubwa kwenye mashindano makubwa huku akishindwa kutwaa taji hata moja mfano; - Fainali ya Euro 2021 - Fainali ya Euro 2024 - Nusu fainali kombe la dunia 2018 - Robo fainali Kombe la dunia 2022
Southgate alijiunga na timu hiyo akitokea timu ya vijana ya Taifa hilo chini ya miaka 21.