pmbet

Spurs watabaki kweli EPL msimu huu?

Sisti Herman

March 23, 2026
Share :

 

Hali ni tete sana kwa upande wa Spurs! Baada ya kipigo cha jana cha 3-0 dhidi ya Nottingham Forest, Tottenham sasa wanapumulia mashine katika harakati za kujinasua na janga la kushuka daraja

Tofauti ya alama kati ya Spurs na West Ham (ambao wako nafasi ya 18) ni alama moja tu. Kuteleza kidogo katika mechi ijayo kunaweza kuwatupa Spurs ndani ya mstari mwekundu.

Baada ya Thomas Frank kufutwa kazi mwezi Februari, kocha mpya Igor Tudor bado hajapata fomula ya ushindi huku mashabiki wakionyesha kutoridhishwa kwa kuzomea uwanjani.

Tangu kuondoka kwa Son Heung-min kwenda LAFC msimu uliopita, Spurs wamekuwa na wakati mgumu kupata mabao ya uhakika, wakitegemea zaidi Richarlison ambaye amefunga mabao 9 pekee msimu huu wa ligi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet