Staa wa ligi kuu Kenya Bajaber kutua Simba.
Joyce Shedrack
July 23, 2025
Share :
Klabu ya Simba inaripotiwa kumalizana na kiungo mshambuliaji hatari wa Kenya Mohamed Bajaber akitokea Police FC ambao ni mabingwa wa ligi kuu Nchini Kenya.

Bajaber mwenye umri wa miaka 22 anasifika kwa uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za magoli huku akipewa matumaini makubwa ya kuwa staa wa Timu ya Taifa ya Kenya.





