Stamina atangaza ngoma saba za album yake mpya.
Joyce Shedrack
November 11, 2024
Share :
Baada ya tarehe 4 Novemba Msanii wa Hip-Hop nchini Stamina kutangaza rasmi juu ya ujio wa Album yake mpya yenye jumla ya nyimbo 17, sasa ametambulisha majina ya nyimbo saba kati ya 17 zilizopo kwenye Album yake hiyo mpya itakayotoka Novemba 14, 2024 aliyoipa jina la "MSANII BORA WA HIP HOP".
Stamina anazidi kuchochea hamu kwa mashabiki zake kwani ndani ya nyimbo hizo alizotoa majina yake amewashirikisha baadhi ya wasanii wakongwe kama vile wagosi wa kaya, Dully sykes, Mwasiti, Linah, Mejja, Belle 9, Kusah pamoja na Jay Rox.
TRACK NO 1 MSANII BORA WA HIP HOP (RMX)
TRACK NO 2 BADO NIPO(FT BELLE 9)
TRACK NO 3 FIRE(FT WAGOSI WA KAYA FT DULLY SYKES)
TRACK NO 4 POMBE MBAYA (FT MEJJA)
TRACK NO 5 LIPEPEWE (FT KUSAH)
TRACK NO 6 KWA UBAYA (FT LINAH)
TRACK NO 7 MAPENZI (FT MWASITI)