Stars mzigoni leo kuwavaa Mongolia FIFA Series 2024
Sisti Herman
March 25, 2024
Share :
Timu ya Taifa Tanzania “Taifa Stars” leo watashuka dimbani kucheza mchezo wa pili wa FIFA Series 2024 dhidi ya timu ya Taifa ya Mongolia mechi itakayopigwa kwenye dimba la Dalga Arena, Azerbaijan mishale ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika mashariki.
Ikumbukwe Stars ambayo ip[o nafasi ya 119 kwenye viwango vya FIFA ilianza kampeni hizi vibaya kwa kupoteza dhidi ya timu ya Taifa ya Bulgaria ambao wapo nafasi ya 83 kwenye viwango vya FIFA.
Mongolia wanaocheza na Stars leo wapo nafasi ya 190 kwenye viwango vya FIFA.