Stars yatoka kwa Mbinde Afcon
Sisti Herman
January 25, 2024
Share :
Baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Congo, Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la Mataifa Afrika AFCON 2023 baada ya kumaliza mkiani mwa Kundi F huku ikikusanya alama 2 kwa kupata sare mbili na kipigo kimoja.
Morocco na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefuzu kwenda hatua ya 16 bora sambamba na wenyeji, Ivory Coast waliofuzu kama ‘best looser’ huku Zambia wakimaliza nafasi ya 3 kwenye kundi, wakiwa sawa na Tanzania, wakitofautiana na idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.