Straika wa magoli aikataa ofa ya Man United
Sisti Herman
June 15, 2025
Share :
Mashine ya Magoli na Straika, Viktor Gyokeres amegomea uhamisho wa kwenda kujiunga na Manchester United, imeripotiwa.
Straika huyo amepania kufanya uhamisho kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huku Arsenal ikiwa moja ya klabu inayotajwa kuisaka kwa nguvu zote saini ya mkali huyo wa kimataifa wa Sweden.
Man United ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kumchukua Gyokeres kutokana na kocha wake Ruben Amorim kufahamiana vyema na mshambuliaji baada ya kumnoa walipokuwa pamoja Sporting CP lakini hali imekuwa tofauti kwenye dili la usajili la mchezaji huyo.