Stumai "Kuchini" hashikiki ufungaji ligi ya wanawake
Sisti Herman
April 21, 2024
Share :
Baada ya jana kufunga goli 5 peke yake kwenye ushindi wa 9-0 dhidi ya Geita Gold Queens, kiungo mshambuliaji wa JKT Queens na timu ya Taifa Tanzania “Twiga Stars” Stumai Abdallah ‘Kuchini’ sasa amefikisha magoli 16 na kuongoza msimamo wa wachezaji wanaoongoza kwa kufunga idadi kubwa ya magoli kwenye ligi kuu wanawake.
Hii hapa orodha ya wachezaji wanne (4) wanaoongoza kwa kufunga magoli mengi;
1. Stumai Abdallah - 16 (JKT Queens)
2. Aisha Mnuka - 13 (Simba Queens)
3. Winifrida Gerald - 8 (JKT Queens)
4. Asha Djafar - 6 (Simba Queens)