Taifa Stars yatinga Ndola kuwavaa Zambia kufuzu kombe la dunia
Sisti Herman
June 9, 2024
Share :
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama ‘Taifa Stars’ kikiongozwa na Kocha Hemed Suleiman, kimewasili mjini Ndola, tayari kuchuana na Zambia kwenye mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026.
Wachezaji hao wanaendelea na mazoezi siku moja baada ya kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Simon Mwansa Kapwepwe.
Mchezo huo wa ugenini kwa Tanzania utachezwa siku ya Jumanne, Juni 11, 2024 ambapo ‘Taifa Stars’ ipo kundi ‘E’ pamoja na Morocco, Congo, Zambia, na Niger.
‘Taifa Stars’ inasaka ushindi muhimu dhidi ya Zambia baada ya kufungwa 2-0 na Morocco mwezi Novemba, 2023 licha ya kupata pointi tatu dhidi ya Niger, ugenini.