Tajiri anunua timu ili yeye na mwanae waweze kupangwa
Eric Buyanza
June 20, 2024
Share :
Mwaka 2021 mfanyabiashara milionea wa kichina aliyefahamika kwa jina la He Shihua alizua minong'ono kwenye mitandao ya kijamii baada ya kununua timu ya daraja la pili iitwayo Zibo Cuju ili yeye na mtoto wake waweze kupangwa tena katika mechi rasmi.
Mjasiriamali huyo anayependa soka, aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kugundua kuwa pamoja na mapenzi ya soka aliyonayo lakini hawezi kuwa mchezaji ambaye angeweza kushiriki mashindano rasmi ya Ligi kwenye timu yoyote ile.
Hata hivyo aligundua kuna njia ya mkato ya kutatua tatizo lake kwa kununua klabu ya soka na kumshinikiza kocha ampange pale timu hiyo inapokuwa na mechi kubwa kubwa.
Tajiri huwa anapangwa kama mshambuliaji na amejivisha mwenyewe jezi namba 10 mgongoni.
Katika hali ya kushangaza kuna siku tajiri aliamka na kumshinikiza kocha ampange kwenye kikosi cha kwanza mtoto wake wa kiume mwenye uzito wa kilo 126.