Tajiri asiyejulikana aagiza ndege 50 kiwandani
Sisti Herman
July 6, 2025
Share :
Kampuni ya kutengeneza ndege za biashara ya Canada - Bombardier imepata agizo la ndege 50 za Bombardier Challenger na Global-family kutoka kwa mteja wa mara ya kwanza ambaye jina lake halikujulikana.
Bombardier inasema mpango huo una thamani ya dola bilioni 1.7, na uwasilishaji unatarajiwa kuanza mnamo 2027.
Zilizojumuishwa katika mkataba huo ni chaguzi za ndege 70 zaidi ambazo, ikiwa zikitekelezwa, zingeongeza thamani agizo hadi wastani wa dola bilioni 4 pamoja na makubaliano ya huduma yaliyoelezewa kama ya kwanza ya aina yake kati ya Mzalishaji na Mwendeshaji.
"Mteja amechagua kutofichua jina lake hadharani," Bombardier ilisema.
Eric Martel, mtendaji mkuu wa Bombardier, anasema agizo hilo "linaonesha faida ya ushindani ya wa bidhaa na huduma za Bombardier kwa wateja katika matumizi ya ndege, kutoka kwa kuundwa hadi uwasilishaji, kisha katika huduma ya ndani ya ndege ".