Tajiri Elon Musk kuburuzwa mahakamani
Eric Buyanza
April 8, 2024
Share :
Jaji wa Mahakama ya Juu ya Brazil, Alexandre de Moraes, ameanzisha uchunguzi dhidi ya mmiliki wa mtandao wa kijamii wa X, Elon Musk.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Musk anatuhumiwa kuzuia sheria kufanya kazi yake, ambapo inaelezwa mmiliki huyo wa mtandao wa X (zamani Twitter) anapingana na uamuzi wa Jaji Moraes ulioutaka mtandao huo wa kijamii kuzifungia baadhi ya akaunti za watumiaji wake.