pmbet

Tajiri Man Utd aomba radhi kwa kauli yake tata kuhusu wahamiaji

Sisti Herman

February 12, 2026
Share :

 

Jim Ratcliffe ametoa taarifa baada ya kukabiliwa na ukosoaji nchini Uingereza na kote Ulaya kuhusiana na maoni yake kuhusu uhamiaji.

Ratcliffe alisema:

"Nasikitika kwamba chaguo langu la lugha limewaudhi baadhi ya watu ... lakini ni muhimu kuzungumzia suala la uhamiaji unaodhibitiwa na kusimamiwa vyema ambao unasaidia ukuaji wa uchumi."

Akiongea katika Mkutano wa Sekta ya Ulaya huko Antwerp, alielezea matamshi yake yalilenga ukuaji wa uchumi, kazi, ujuzi na utengenezaji sio mgawanyiko.

Aliongeza:

"Serikali lazima zidhibiti uhamiaji pamoja na uwekezaji katika ujuzi, viwanda na kazi ili ustawi wa muda mrefu ushirikiwe na kila mtu."

Ratcliffe alisisitiza umuhimu wa kudumisha "mjadala wazi juu ya changamoto zinazoikabili Uingereza."

Ufafanuzi lakini utatuliza maoni kutoka kwa umma ... binafsi hapana haifai kwa sababu unapaswa kuwajibika kwa maneno yako!

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet