pmbet

Tajiri namba 3 duniani awekeza Liverpool zaidi ya Trilioni 2

Eric Buyanza

August 15, 2026
Share :

Fenway Sports Group (FSG) imetangaza rasmi kuuza sehemu ndogo ya hisa za Liverpool kwa muungano wa wawekezaji unaoungwa mkono na bilionea maarufu Jeff Bezos.

 

Bezos amewekeza zaidi ya dola bilioni 1 (sawa na takriban Shilingi trilioni 2 na bilioni 647 za Tanzania), hata hivyo yeye atakuwa mwekezaji tu na hatakuwa na kiti kwenye bodi ya wakurugenzi ya Liverpool kwa sasa.

 

Uwekezaji huo kupitia 1892 Holdings unalenga kusaidia Liverpool katika mipango yake ya ukuaji wa muda mrefu, ndani na nje ya uwanja. 
Liverpool inaendelea kujiimarisha kibiashara na kisporti kwa ajili ya mafanikio ya muda.

 

Licha ya kuingia kwa wawekezaji wapya, muundo wa umiliki wa Liverpool hautabadilika kwa kiasi kikubwa, huku FSG ikithibitisha kuwa itaendelea kuwa na umiliki wa hisa nyingi pamoja na udhibiti wa uendeshaji wa klabu.

 

Wawekezaji hao kutoka kwenye muungano huo watafanya kazi kwa karibu na FSG pamoja na uongozi uliopo wa Liverpool.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet