Tajiri United aifananisha Man Utd na Coca-Cola
Sisti Herman
June 20, 2024
Share :
Tajiri wa Uingereza Sir Jim Ractliffe ambaye anamiliki hisa asilimia 25 kwenye klabu ya Manchester United kupitia kampuni ya INEOS kwenye mahojiano yake maalumu na Bloomberg ameifananisha klabu ya Man Utd kwa umaarufu na kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola.
"Kila mtu duniani anaijua Manchester kwasababu ya Manchester United, tunaweza kusema Manchester United ni kama Coca-cola, kila mtu anaijua" alisema tajiri huyo.
"Tunahitaji kuwa sehemu waliopo Real Madrid japo itachukua muda mrefu kidogo, tunahitaji madirisha ya usajili kama mawili hadi matatu kuwa na timu bora" alimaliza tajiri huyo.