Tajiri United aweka masharti matano mezani
Sisti Herman
May 30, 2024
Share :
Bilionea wa Uingereza ambaye amenunua hisa asilimia 25 kwenye klabu ya Manchester United zinazomfanya kuwa na nguvu zaidi kuendesha shughuli za mpira kwenye klabu hiyo Sir Jam Ratcliffe ametoa masharti makubwa matano kwaajili ya Operesheni ya kendesha klabu hiyo.
Haya hapa ni masharti hayo ambayo anaamini yatawezesha United kurejea kwenye makali yake;
1. Umri wa juu wa wachezaji watakaosajiliwa ni miaka 25.
2. Hakuna kusajili mastaa wenye majina makubwa.
3. Staili ya uchezaji itaamuliwa na mkurugenzi wa ufundi, Jason Wilcox.
4. Kocha ataomba nafasi gani ya mchezaji anayetaka asajiliwe na si kutaka mchezaji fulani.
5. Kocha atapewa majina matatu ya kila nafasi anayotaka mchezaji asajiliwe, atachagua mmoja.
Bilionea Ratcliffe anaamini kusajili wachezaji wenye umri wa miaka 25 kushuka chini watafanya kikosi kuwa fiti, chenye nguvu na kasi kubwa uwanjani.
Bosi huyo hataki tena kusajili mastaa wenye majina makubwa kwa sababu hakuna ambacho wamefanya kwenye timu zaidi ya kuipa timu gharama kubwa kwenye matumizi ya pesa.
Man United imetumia Pauni 1.5 bilioni kwenye usajili wa mastaa wapya tangu Sir Alex Ferguson alipong'atuka 2013.