Taliban wanataka kubadilishana wafungwa na Marekani
Eric Buyanza
July 3, 2024
Share :
Serikali ya Taliban ya nchini Afghanistan imeonyesha nia ya kuwaachilia wafungwa wawili raia wa Marekani kwa kubadilishana na raia wa Afghanistan wanaoshikiliwa Marekani.
Msemaji mkuu wa serikali ya Taliban, Zabihullah Mujahid, amewaambia waandishi wa habari mjini Kabul kwamba swala la kuwaachilia huru wafungwa limejadiliwa wiki hii katika mkutano na maafisa wa Marekani mjini Doha.