pmbet

Tamasha la Wanyakyusa kufanyika Dar Julai 26-27

Eric Buyanza

March 26, 2024
Share :

Katibu Mkuu Mstaafu Wizara ya Ujenzi, Elius Mwakalinga, amewaita watu wenye jamii ya kinyakyusa kuungana pamoja katika kufanikisha tamasha la siku yao linalotarajiwa kufanyika Julai 26 hadi Julai 27 mwaka huu.
 

Mwakaliga ametoa wito huo jijini Dar es Salama alipokutana na wanyakyusa kutoka sehemu mbalimbali katika kikao maalumu kwa lengo la kuchangia na kuweka mikakati ya kufanikisha tamasha hilo.
 

Mstaafu huyo amesema tamasha hilo halina lengo la kuonyesha ukabila na kwamba linalengea kuenzi tamaduni zao za asili.
 

“Gharama za sherehe kwa muujibu wa bajeti iliyopangwa ni Shilingi milioni 371, pesa hizi ni nyingi sana, lakini nimeambiwa mpaka sasa kuna zaidi ya wanyakyusa 1,000 wamejiunga kwenye group la ‘whatsap’ na bado wanaongezeka idadi hii ni kubwa sana na inatia moyo”
 

“Mimi kwa leo nimeanza kwa kutoa Sh milioni 2 nitakuwa ninaendelea kuchanga kila siku kadri siku zinavyozidi kusonga mbele” amesema Muhandisi Mwakalinga.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet