TAMISEMI yaomba kuidhinishiwa Bajeti ya Sh 10 Trilioni 2024/25
Sisti Herman
April 16, 2024
Share :
Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imeliomba Bunge likubali kuidhinisha Sh10.1 trilioni ambazo ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa wizara hiyo.
Fedha hizo ni ongezeko la Sh981 bilioni ikilinganishwa na fedha zilizoombwa na wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24, kiasi cha Sh9.1 trilioni.
Waziri wa Tamisemi, Mohamed Mchengerwa ametoa maombi hayo bungeni leo Jumanne Aprili 16, 2024 wakati akisoma makadirio ya mapato na mtumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25, yanayohusisha mafungu ya Tamisemi, Tume ya Utumishi wa Walimu na mikoa inayojumuisha halmashauri 184.
Mchengerwa amesema fedha hizo zinahusisha Sh3.4 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo kati ya hizo, Sh2.2 trilioni ni fedha za ndani na Sh1.1 trilioni ni fedha za nje.