Tanesco watoa ufafanuzi hitilafu ya umeme, wasisitiza uvumilivu
Sisti Herman
April 1, 2024
Share :
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa ufafanuzi kuhusu kitendo cha kukatika kwa umeme kuanzia saa nane usiku wa kuamkia leo katika mikoa mbalimbali Nchini pamoja na Visiwani Zanzibar.
Taarifa ya TANESCO kwa umma imesema majira ya saa nane na dakika 22 alfajiri kuamkia leo April 1 2024 kumetokea hitilafu kwenye gridi ya Taifa na kupelekea Mikoa yote ambayo imeunganishwa na gridi hiyo kukosa umeme.
“Wataalamu wetu tayari wamekwishaanza kufanya jitihada za kuhakikisha kwamba wanarejesha nishati ya umeme kwenye Mikoa yote iliyoathirika, tunaomba sana Watanzania wote kuwa na uvumilivu wakati tunaendelea na jitihada za kurejesha huduma ya umeme” ilisema taarifa ya Tanesco kwa umma.