Tanzania-Burkina Faso kushirikiana kwenye sekta ya afya
Eric Buyanza
May 24, 2025
Share :
Ubalozi wa Tanzania Abuja nchini Nigeria umefanikisha ziara ya ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka Burkina Faso iliyofanyika tarehe 19 hadi 23 Mei, 2025 jijini Dar es Salaam.
Burkina Faso ni miongoni mwa nchi za zilizopo katika eneo la uwakilishi la Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria.
Kupitia ziara hiyo Tanzania na Burkina Faso zimesaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma bobezi za matibabu ya magonjwa ya moyo.
Hati hiyo imesainiwa tarehe 22 Mei, 2025 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge na Mshauri wa Rais wa Burkina Faso na Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Afya wa Rais, Bwana Drissa Traore.