pmbet

Tanzania kupokea ugeni mzito siku ya kesho.

Joyce Shedrack

June 20, 2024
Share :

Rais Jamhuri ya Guinea Bissau, Umaro Sissoco Embaló anatarajia kufanya ziara ya siku tatu Nchini Tanzania yenye lengo la kuimarisha uhusiano na diplomasia kati ya Tanzania na Taifa hilo.

Ziara hiyo inayotarajiwa kuanza kesho Ijumaa Juni 21 hadi Juni 23 italenga maeneo ya kushirikiana katika sekta mbalimbali za kimkakati ikiwemo kutembelea miradi mbalimbali ya uzalishaji nchini pamoja na kutembelea mradi wa Reli ya Umeme (SGR).
 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Dk Samwel Shelukindo amesema kupitia ziara ya Rais Embaló, Tanzania na Guinea Bissau zimedhamiria kuimarisha na kuinua kiwango cha ufanyaji biashara na uwekezaji hasa kupitia Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet