Tanzania kuwa kati ya nchi 20 zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani
Eric Buyanza
February 15, 2024
Share :
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) mwaka huu, Tanzania inatarajiwa kuwa kati ya nchi 20 zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus, Rais Samia amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wawekezaji wa Norway kuja Tanzania kwa kuwa nchi pia ina mazingira mazuri ya kisiasa, kijiografia na kiuchumi.
Akihutubia Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya nchi hizo mbili uliofanyika jijini Oslo, Rais Samia alisema zipo kampuni kadhaa za Norway zilizotumia fursa hiyo vizuri kwa uchumi wa Tanzania.