pmbet

Tanzania kuwa Nchi ya kwanza Afrika kufanya filamu na Korea Kusini.

Joyce Shedrack

July 5, 2024
Share :

Tanzania inatarajia kuwa Nchi ya kwanza Afrika kufanya filamu (movie) kwa kushirikiana na wasanii wakubwa wa Nchi ya Korea Kusini.

Rais wa filamu wa nchi hiyo YANG Jongkon amethibitisha hilo wakati akizungumza na waigizaji kutoka Tanzania katika mji wa Busan unaoongoza kwa filamu duniani ikiwa ni siku ya tatu wakiwa katika ziara ya kujifunza soko la filamu nchini Korea kusini iliyoandaliwa na Rais wa Samia Suluhu Hassan.

Yang Jongkon amesema “Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuunganisha soko la filamu la Tanzania na Korea basi nami sina budi kusema wazi kuwa Tanzania ndio nchi ya kwanza tutakayoshirikiana nayo tutakapoingia Afrika. Kwa sasa tunamalizia kuimarisha bara la Asia kwenye tasnia hii ya filamu”.

Aidha,Jongkon ameahidi kuja Tanzania kuonana na wasanii wa Tanzania akiongozana na baadhi ya watengeneza filamu wa Korea.

Wasanii kutoka Tanzania wamefanikiwa kutembelea Studio kubwa za Busan na kuona jinsi filamu za kikorea ambazo zimetokea kupendwa sana na watanzania zinavyotengenezwa. Filamu hizi maarufu zinazotambulika kama Kdrama(Korean drama) zimetokea kuiteka dunia na kuiweka Korea juu kabisa katika masoko ya filamu kimataifa.

Kiongozi wa msafara huo wa wasanii Steve Nyerere alimkabidhi Rais wa Filamu wa Nchi hiyo zawadi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet