Tanzania na Kenya zaondoa vikwazo vya kibiashara
Sisti Herman
March 24, 2024
Share :
Jumuiya ya Mkutano wa Kamati ya Nane ya Pamoja ya Biashara (JTC) kati ya Kenya na Tanzania kushughulikia masuala yanayoathiri biashara imeondoa vikwazo kadhaa vya Kibiashara ikiwemo Uondoaji wa mbao kutoka Tanzania katika eneo la Lunga Lunga/Horohoro zilizokuwa zimezuiliwa na Shirika la Viwango la Kenya
Maamuzi mengine yaliyofikiwa katika Mkutano huo uliofanyika Kisumu, Kenya, Machi 18 hadi 22, 2024 ni kurejesha mauzo ya chai kwenda Tanzania na kusafisha ‘spirit’ (Konyagi) iliyokuwa imekwama Namanga baada ya kuzuiwa na Shirika la Viwango la Kenya
Mkutano huo ulifanyia kazi na kupata utatuzi wa masuala 14 (6 kutoka Tanzania, 8 kutoka Kenya), kukubaliana uwianishaji wa jumla wa Tozo, Ada na masharti mengine yanayoathiri biashara kati ya Nchi hizo na wamekubaliana Mkutano unaofuata utafanyika Julai 2024 Nchini Tanzania