Tanzania, Uganda kuanza usafirishaji wa Mafuta ghafi February 2026
Sisti Herman
September 22, 2026
Share :

Tanzania na Uganda zinatarajiwa kuanza usafirishaji wa kwanza wa mafuta ghafi kupitia Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) mwezi Februari 2027, hadi sasa ujenzi wa bomba hilo umefikia asilimia 92.7.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame, amesema zoezi la kujaza mafuta kwenye bomba hilo litaanza Disemba 2026, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kuanza kwa usafirishaji wa mafuta kwenda Tanga.
Makame, ameongeza kuwa meli ya kwanza ya kusafirisha mafuta ghafi inatarajiwa kuondoka Tanga Februari au mwanzoni mwa Machi 2027.
EACOP ina urefu wa kilomita 1,443 na itasafirisha mafuta kutoka maeneo ya uzalishaji nchini Uganda hadi Kituo cha Chongoleani Marine Terminal, Tanga, kwa ajili ya kusafirishwa kwenda masoko ya kimataifa.
Mradi huo wenye thamani ya takriban Dola bilioni 5 unatarajiwa kudumu kwa miaka 25.





