pmbet

Tanzania yashinda nafasi ya kuandaa tuzo za Utalii Duniani

Sisti Herman

May 19, 2025
Share :

Tanzania meshinda nafasi ya kuwa mwenyeji wa Tuzo za Utalii Duniani (World Travel Awards) kwa Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi, tukio litakalofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 28 Juni, 2025.

 



Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, kuwa mwenyeji wa tukio hili kunatarajiwa kuongeza hadhi ya nchi, kuimarisha utalii wa mikutano, na kuvutia wawekezaji wapya kwenye sekta hiyo.

“Tanzania imeendelea kung’ara kwa kushinda Tuzo mbalimbali za utalii katika nyanja za Kimataifa zikiwemo zile mashuhuri zaidi duniani katika sekta ya utalii ziitwazo World Travel Awards (WTA), ambapo katika mwaka mmoja uliopita Tanzania imeibuka kinara,” amesema Waziri wa Utalii na Maliasili, Balozi Pindi Chana

Baadhi ya tuzo muhimu ni pamoja na Tuzo ya Dunia kuwa Eneo linaloongoza Duniani kwa utalii wa Safari (World’s Leading Safari Destination, 2024); Tuzo ya kuwa Eneo Linalovutia zaidi kiutalii Afrika (Africa’s Leading Destination, 2024);

Hifadhi ya Taifa Serengeti kuendelea kuwa Hifadhi Bora Duniani kwa miaka sita (6) mfululizo kuanzia mwaka 2019 hadi 2024 (Leading National Park, 2019-2024); na Mlima Kilimanjaro kuwa Kivutio Bora cha Utalii Barani Afrika (African Leading Tourism Attraction, 2024).


 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet