pmbet

Tanzania yashuka nafasi 2 kwenye viwango vya FIFA

Sisti Herman

April 2, 2026
Share :

 

Tanzania imeporomoka hadi nafasi ya 113 duniani toka ile ya 110, kwa ubora soka, kulingana na orodha mpya iliyotolewa na FIFA, Aprili 1, 2026.

Tanzania ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Liechtenstein kwenye michuano ya FIFA Series iliyofanyika hivi karibuni nchini Rwanda, licha ya baadaye kuja kuifunga Macau, bao 6-0.

Kwa upande wao, Kenya wamepanda kwa nafasi mbili kwenye orodha ya FIFA, kutoka ya 113 hadi 111 duniani, baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya Grenada kwenye michuano hiyo hiyo.

DRC, ambayo imetoka kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka 2026, imeendeleza ubabe wake wa soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ikishika nafasi ya 46 duniani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet