pmbet

Tanzania yavunja rekodi ya kupunguza vifo mama na mtoto

Eric Buyanza

June 25, 2024
Share :

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya mama na mtoto kabla ya muda uliotegemewa na kuvunja rekodi ya kufikia 104 badala ya 225 iliyotegemewa mwaka 2025.

Dkt. Mollel, ameeleza hayo leo Jumatatu June 24, 2024 bungeni, Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tasca Mbogo, ambaye alihoji kuwa  Serikali ina mkakati gani wa kupunguza vifo vya Mama na Mtoto katika Mkoa wa Katavi ambako kuna ongezeko kubwa kwa sasa.

Dkt. Mollel amesema Kitaifa vifo vimepungua kutoka 556 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 104 mwaka 2023 ambapo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ilitegemewa vifo vipungue hadi  kufikia 225 ifikapo mwaka 2025.

Amesema, kwa mujibu wa takwimu za Mfumo wa Utoaji Taarifa za Afya (MTUHA) vifo vitokanavyo na uzazi unaonesha kwamba, tangu mwaka 2020 hadi 2024 mtiririko wa vifo vya akina mama Mkoani Katavi ni kama ifuatavyo Mwaka 2020 vifo 56,mwaka 2021 vifo 41, mwaka 2022 vifo 36, mwaka 2023 vifo 33, na mwaka 2024.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet