Tanzanite Princess yatwaa Ubingwa Ligi ya wanawake mkoa wa Dar es Salaam
Sisti Herman
April 8, 2026
Share :

Timu ya Tanzanite Princess wametawazwa rasmi kuwa Mabingwa wa michuano ya Ligi ya Mabingwa wa soka la wanawake mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuifunga timu ya Wisdom Queens goli 10-0.
Tanzanite Queens wamekuwa mabingwa baada ya kumaliza ligi wakiwa na alama 12 juu ya Mbagala Queens na Rangi tatu Queens waliomaliza wakiwa na alama 10 na 9.
Mchezo wa awali uliwakutanisha Mbagala Queens na Rangi 3 Queens waligawana alama baada ya kutoka sare ya 1-1.
Wachezaji walioshinda tuzo binafsi;
1. Mfungaji bora - Fatuma Muhibu akiwa na tuzo yake
3. Kipa bora -Leila Juma akiwa na tuzo yake
4. Mabingwa rasmi - Tanzanite Princess FC





