Tanzanite Queens kuikabili Brazil kombe la Dunia.
Joyce Shedrack
September 5, 2026
Share :
Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite Queens, leo inaingia uwanjani nchini Poland kuikabili Brazil katika mchezo wa Kombe la Dunia la Wanawake U20.
Mchezo huo ni sehemu ya safari ya Tanzanite Queens katika mashindano hayo makubwa ya dunia, ambapo timu hiyo imebeba jukumu la kuiwakilisha Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa.
Msemaji wa Timu za Taifa, Haji Manara, amewasihi Watanzania kuendelea kuipa sapoti timu hiyo pamoja na kuwaombea wachezaji ili wafanye vizuri na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Manara amesema ushirikiano, hamasa na sapoti kutoka kwa Watanzania ni muhimu kwa Tanzanite Queens katika kipindi hiki ambacho inaiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya dunia.





