pmbet

TANZIA, Mwigizaji mkongwe wa Hollywood afariki dunia.

Joyce Shedrack

June 21, 2024
Share :

Mwigizaji wa Hollywood Donald Sutherland, kutoka nchini Canada aliyejizolea umaarufu kupitia filamu ya  ‘The Hunger Games’ na MASH, amefariki dunia siku ya jana  nyumbani kwake jijini Miami,Florida nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 88 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mtoto wa mwigizaji huyo Keifer Donald ambaye pia ni mwigizaji amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake huku akieleza namna alivyosikitishwa na msiba huo. 

Keifer amesema “Kwa moyo mzito, ninatangaza kwamba baba yangu, Donald Sutherland, ameaga dunia. Binafsi nadhani mmoja wa waigizaji muhimu katika historia ya filamu, lipenda alichofanya na kufanya kile alichopenda” 

 

Sutherland aliwavutia mashabiki wengi kupitia  filamu za kivita alizoigeza na kuonesha umahiri mkubwa zikiwemo ‘Kelly's Heroes’,  na ’‘The Eagle Has Landed’ .

Mwigizaji huyo alikabidhiwa tuzo ya nyota ya heshima ya ‘The Hollywood Walk Of Fame’ mwaka 2011 kutokana  na mchango wake wa kukuza tasnia ya uigizaji nchini Marekani.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet