Tarehe 21 Julai imezaa kumbukumbu mbaya kwa Makamba mara ya pili.
Joyce Shedrack
July 22, 2024
Share :
Tarehe 21 mwezi wa 7 inaingia kwenye historia ya Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba kuwa siku yenye historia mbaya kwenye maisha yake ya kazi kutokana na tarehe hiyo hiyo na mwezi huo kutenguliwa mara mbili kuwa Waziri na Marais wawili tofauti.
Tarehe 21 mwezi wa 7 mwaka 2019, Makamba alitenguliwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli kuwa waziri wa nchi ofisi ya makamu wa raisi muungano na mazingira na nafasi yake ilichukuliwa George Simbachawine .
Siku ya Jana tarehe 21 mwezi wa 7 2024, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua Uteuzi wa January Makamba aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki huku nafasi yake ikichukuliwa na Balozi Mahmoud Kombo ambaye alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.