Tatizo la upweke laongezeka kwa vijana wa Afrika - Tafiti
Eric Buyanza
September 9, 2025
Share :
Utafiti uliofanywa mwaka 2023 na taasisi ya maoni ya Gallup kwa kushirikiana na kampuni mama ya Facebook, Meta, ulibaini kati ya nchi 29 duniani zilizo na viwango vya juu vya upweke, 22 zipo barani Afrika.
Utafiti huo unaakisi kukua kwa tatizo la upweke miongoni mwa vijana hasa wanaotoka katika mataifa masikini.
Katika utafiti huo watu 1,000 walihojiwa kwenye mataifa 142. Kati ya nchi 29 zilizobainika kuwa na viwango vya juu vya upweke ishirini na mbili zinatoka barani Afrika. Utafiti huu unaungwa mkono na ule uliofanywa na Shirika la Afya Duniani WHO mnamo mwaka huu wa 2025, ukionesha wazi kuwa watu wanaoishi katika nchi maskini wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kukumbwa na upweke, na vijana ndio wanaoathirika zaidi.
"Hili si tatizo la Ulaya na Marekani pekee au mataifa tajiri pekee, upweke ni tatizo la kidunia." Anasema Julianne Holt- Lunstad mshauri wa kitaaluma wa utafiti huo akiongeza kuwa tatizo hilo halionekani kupewa kipaumbele barani Afrika.