pmbet

TAWA yasaini mikataba ya uwekezaji mahiri yenye thamani Bil 719

Sisti Herman

August 13, 2025
Share :

 

Katika hatua ya kihistoria na kishindo kwa sekta ya utalii nchini, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), leo Agosti 12, 2025, imesaini mikataba minne ya uwekezaji wa utalii kupitia utaratibu wa Uwekezaji Mahiri (SWICA) na kampuni ya kitanzania ya Uhusiano International ICT Ltd.

Mikataba hiyo inatarajiwa kuingiza mapato ya Dola za Marekani milioni 281.5 (sawa na Shilingi Bilioni 719 za Kitanzania) kwa kipindi cha miaka 20 ikiwa ni wastani wa Shilingi Bilioni 36 kwa mwaka.

Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam na imehusu uwekezaji katika vitalu vinne vya Burko Open Area (Monduli – Arusha), Selous MHJ1, Selous MHJ2 na Selous ML1 (Liwale – Lindi), vyote vikiwa chini ya kampuni ya Uhusiano International ICT Ltd inayomilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana amesema uwekezaji huo utaimarisha sekta ya uwindaji wa kitalii na utalii wa picha, sambamba na kuleta ajira, kuboresha huduma za jamii na kuchochea maendeleo ya wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya uwekezaji. Miradi ya maendeleo itakayoibuliwa na wananchi wenyewe inakadiriwa kugharimu Dola milioni 1.8 (sawa na Shilingi Bilioni 4.6) kwa miaka 20.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana aliahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kusisitiza umuhimu wa matumizi endelevu ya rasilimali kwa kuzingatia sheria, kanuni na misingi ya uhifadhi bora. Alitoa wito kwa wawekezaji zaidi kuja kuwekeza katika vivutio vya kipekee vya utalii vilivyopo nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis R. Semfuko, amesema TAWA imepiga hatua kubwa kwa kusaini mikataba minne mipya ya SWICA na kufikisha jumla ya mikataba 13 kati ya 14 iliyopangwa sawa na asilimia 92.3 ya lengo, hatua iliyowezesha kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 27.4 kati ya Januari 2024 na Agosti 2025.

Aidha, Meja Jenerali Semfuko alibainisha kuwa TAWA ipo katika hatua

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet