Tayari Chelsea wamaliza, wajiokotea kinda Omari Kellyman kutoka Aston Villa
Eric Buyanza
June 29, 2024
Share :
Chelsea wamekamilisha usajili wa mshambuliaji kinda kutoka Aston Villa, Omari Kellyman kwa mkataba wenye thamani ya pauni milioni 19.
Dili hilo limekamilika baada ya Chelsea kutangaza leo Jumamosi asubuhi kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 amesaini mkataba wa miaka sita na klabu hiyo .
Omari alijiunga na Villa mwaka wa 2022 akitokea Derby County.