Taylor Swift ameza mdudu akitumbuiza mbele ya mashabiki
Eric Buyanza
June 25, 2024
Share :
Mwanamuziki wa Marekani Taylor Swift kwa bahati mbaya alimeza mdudu siku ya Jumapili wakati alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha lake la "Eras" jijini London.
Taylor alijikuta amemeza mdudu wakati alipokuwa akiimba wimbo wa ‘All Too Well.’
Alikuwa amesimama akipiga gitaa lake na kuimba na mara ghafla akatangaza hadharani kuwa amemeza mdudu, na kuwataka mashabiki waendelee kuimba.
Ingawa Taylor alijitahidi kuendelea lakini alikwama na kuanza kukohoa.