Taylor Swift avunja rekodi ya Dunia!
Eric Buyanza
December 15, 2023
Share :
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Taylor Swift kwa sasa ndiye anayepata pesa nyingi katika show za muziki ambapo ziara yake ‘The Eras Tour’ imeingia kwenye Kitabu cha Kumbukumbu za dunia ‘Guinness World Records’ kwa kuwa ziara iliyoingiza pesa ndefu zaidi kwa muda wote.
Ziara hiyo imeingiza kiasi cha Dola 1.04 bilioni zaidi ya Tsh. 2.5 trilioni kwenye matamasha 60 ambayo ameyafanya hadi sasa kwenye maeneo mbalimbali duniani.
Pia ziara hiyo ina jumla ya maonesho 151 hivyo bado maonesho 91 kukamilisha mzunguko wote ambao ulianza March 17, 2023 na utamalizika Disemba 8, 2024.