Tazama Darwin Núñez wa Liverpool, akizichapa 'kavukavu' na mashabiki
Eric Buyanza
July 11, 2024
Share :
Nyota wa Liverpool Darwin Núñez ni miongoni mwa walioonekana wakiwachapa ngumi mashabiki ikiwa ni muda mchache baada ya timu yake ya taifa ya Uruguay kutandikwa na Colombia 1-0 kwenye mchezo uliochezwa alfajiri ya leo.
Núñez alionekana akiwakabili mashabiki hao wa Colombia baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa katika nusu fainali ya mashindano ya Copa America.