Tchouameni amtaja Davido kama msanii wake bora
Eric Buyanza
January 10, 2024
Share :
Kiungo wa Real Madrid Aurelien Tchouameni amemtaja msanii wa Nigeria David Adeleke (Davido), kama msanii wa Afrobeats anayemhusu zaidi.
Mchezaji huyo raia wa ufaransa ameyasema hayo kwenye mahojiano kwenye kipindi cha 'Kick Game UK' alipoulizwa na muendeshaji wa kipindi hicho kuwa yupi ni msanii Afrobeats anayemkubali?
Tchouameni akajibu: “Davido, huyo ndio mtu wangu.”