pmbet

Tembo FC waahidiwa million 1.5 kumuuwa Simba SC

Joyce Shedrack

January 31, 2024
Share :

Michuano ya kombe la Shirikisho Azam (ASFC) inaendelea tena leo Januari 31, 2024 kwa mchezo mmoja wa hatua ya 32 bora ambapo Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watakuwa kibaruani dhidi ya Tembo FC ya Mkoani Tabora katika dimba la Azam Complex, Chamazi majira ya saa 1:00 jioni.

 

Simba SC watarejea leo uwanjani kutafuta ushindi wa kwanza utakaowawezesha kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hii baada ya mtani wao Yanga SC kufuzu hatua hiyo jana kwa kishindo kwa kuitandika Hausung ya Njombe magoli 5 kwa 1.

 

Pamoja na kukiri kuzidiwa na Simba, Tembo FC imesema inahitaji rekodi ya kuwafunga wapinzani wao hao bila kujali matokeo ya jumla ili kuandika historia, huku mabosi wakitangaza dau la Sh1.5 milioni kwa kila bao litakalopatikana kuhakikisha Mnyama anakufa mapema.

 

"Sisi ni Tembo, wao ni Simba ina maana wanyama wakali msituni tunakutana. Uongozi umeweka mipango mizuri na kuonyesha tunaitaka hiyo mechi tutanunua kila bao Sh1.5 milioni. Tumewaambia wachezaji wapambane tuweke historia," amesema Yusuph. 

 

Timu hiyo kongwe ambayo haishiriki ligi yoyote iliyoanzishwa 1987 ikiwa chini Halmashauri ya Nzega kabla ya kurejeshwa kwa wananchi, inakutana na Wekundu wa Msimbazi kwa mara ya kwanza katika historia mchezo ambao utapigwa jijini Dar es Salaam. 

 

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ramadhan Kilobi amesema wanafahamu Simba ni timu kubwa ndani na nje ya uwanja, lakini hawataingia kinyonge badala yake watapambana kutafuta matokeo mazuri.
 

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet