pmbet

Tems ajiunga na umiliki wa klabu inayoshiriki ligi kuu Marekani.

Joyce Shedrack

February 13, 2025
Share :

Mwanamuziki nyota wa Nigeria, Tems, mshindi wa tuzo ya Grammy, amejiunga rasmi na San Diego FC kama mshirika wa umiliki. Kupitia tangazo rasmi, alionekana akivalia jezi ya klabu hiyo, hatua iliyopokelewa kwa shangwe na mashabiki wake kote ulimwenguni.

Tems anaungana na wasanii wengine wanaowekeza katika michezo, na ushirikiano wake unatarajiwa kuongeza mvuto wa kimataifa kwa San Diego FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS). 

 

Hatua hii inaonyesha muunganiko kati ya muziki na michezo, ikifungua ukurasa mpya katika safari yake ya uwekezaji.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet