Tems aongoza Sound Track ya filamu anayocheza Ayra Starr.
Joyce Shedrack
July 29, 2026
Share :
Msanii wa Nigeria, Tems, ametangazwa rasmi kuwa mtayarishaji mkuu (Executive Producer) na msimamizi wa soundtrack ya filamu inayotarajiwa kwa hamu, Children of Blood and Bone.
Mkurugenzi wa filamu hiyo, Gina Prince-Bythewood, amesema Tems ndiye aliyeongoza mchakato wa kuandaa soundtrack hiyo, akikusanya nyimbo tatu mpya kutoka kwake pamoja na kazi za Burna Boy, Fireboy DML, BNXN na Ayra Starr.
Mbali na hilo, Burna Boy amejiunga na project hiyo kama mshauri mkuu wa masuala ya muziki (Executive Music Consultant), akisaidia kuhakikisha soundtrack hiyo inakuwa na ubora wa hali ya juu.
Filamu ya Children of Blood and Bone inatarajiwa kuonyeshwa rasmi mwezi Januari 2027, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona na kusikia kazi hiyo mpya.





