pmbet

Ten Hag ataja wachezaji 5 watakaorejea kikosini Januari

Eric Buyanza

December 30, 2023
Share :

Meneja wa Manchester United, Erik Ten Hag ameorodhesha wachezaji watano ambao wanatarajiwa kurejea kutoka kwenye majeraha mwezi Januari.
 

Ten Hag alikuwa akitoa taarifa za timu kabla ya mchezo wao dhidi ya Nottingham Forest leo (Jumamosi).
 

Mashetani Wekundu kwa sasa wako nafasi ya saba kwenye ligi huku wakikabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Tottenham Hotspur na Aston Villa katika michezo yao mitano ijayo ya ligi kuu.
 

"Katikati ya Januari tunatarajia wachezaji wengi kurudi. Mason Mount, Casemiro, Lisandro Martinez, Tyrell Malacia.

"Tunatarajia pia Harry Maguire, bila shaka. Tunatarajia wachezaji wengi kurejea Januari,” Ten Hag aliwaambia wanahabari.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet