Ten Hag na Rashford yameisha
Sisti Herman
February 1, 2024
Share :
Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amethibitisha kuwa klabu hiyo imemuwajibisha mshambuliaji wao Marcus Rashford kwa makosa ya kinidhamu wikiendi iliyopita, yameisha na sasa amejiunga na wenzake kwaajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Wolves.
“Hatukuambatana naye jumapili (mchezo uliopita), yalikuwa ni masuala ya kinidhamu na ameshawajibishwa, mengine ni mambo ambayo yanatakiwa yaishie ndani ya timu, tutakuwa naye dhidi ya Wolves”
Rashford alikumbana na adhabu nzito ya kukatwa mshahara zaidi ya bilioni 2 za kitanzania baada ya kunaswa akiwa sehemu za starehe siku 1 kabla ya mchezo wa ligi wkiendi iliyopita.