TETESI: Ronaldo kuitupa Al Nassr, kutimkia Brazil
Eric Buyanza
May 27, 2025
Share :
Cristiano Ronaldo amechapisha ujumbe usioeleweka kuhusu mustakabali wake siku chache baada ya rais wa FIFA Gianni Infantino kusema kuna majadiliano yanafanyika ili fowadi huyo acheze kwenye Kombe la Dunia la Vilabu.
Ronaldo kwa sasa anachezea klabu ya Al Nassr ya Saudia, ambayo ilishindwa kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu ambalo litashirikisha timu 32 msimu huu nchini Marekani.
Ronaldo ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni wa mwezi Juni, angehitaji aweze kuachiliwa mapema ili aweze kusaini klabu inayoshiriki Kombe la Dunia la Vilabu, ambalo litaanza Juni 14.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ronaldo aliandika:
"Sura hii imekwisha. Hadithi? Bado inaandikwa. Asante kwa wote."
Botafogo, Fluminense, Flamengo na Palmeiras ndizo timu za Brazil zitakazoshiriki michuano hiyo.