Tetesi za Seleman Mwalimu zamuibua Ally Kamwe.
Joyce Shedrack
April 18, 2026
Share :
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya @yangasc Ally Kamwe amefunguka kuhusu tetesi zilizokuwa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamiii kwamba klabu hiyo imefanya mazungumzo na Wydad AC ili kuhitaji saini ya mshambuliaji wa Wydad na Simba Seleman Mwalimu.
Semaji la Wananchi amekanusha taarifa hizo huku akiweka wazi kuwa ni taarifa za uzushi na viongozi wanashughulikia suala la wachambuzi wanaongea na kuandika habari zenye lengo la kuichafua Yanga.

"Uongozi wa Young Africans Sports Club Haujafanya mazungumzo na Klabu/Mtu yoyote kuhusu kumuhitaji mchezaji Seleman Mwalimu.
"Hizi ni Taarifa za uzushi na hazina ukweli wowote. Mawakala/Wachambuzi tumieni mbinu nyingine ya kuwatafutia Mikataba wachezaji wenu, Hii ya kuitumia Yanga imetosha sasa.
"Nb: Kuhusu Wachambuzi wanaoandika/Kuongea Habari zenye lengo la kuichafua Klabu ya Yanga, viongozi wanashughulikia jambo hilo na muda sio mrefu nitawajuza hatua zitakazochukuliwa.
“Daima Mbele Nyuma Mwiko”.Ameandika Ally Kamwe.





