TETESI ZA SOKA: Arsenal vitani na Manchester United kuwania saini ya Mikayil Faye
Eric Buyanza
April 5, 2024
Share :
Arsenal wanajiandaa kupambana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki kinda wa Barcelona mwenye umri wa miaka 19 Mikayil Faye.
Arsenal wanahisi mlinzi huyo anayetumia mguu wa kushoto ana sifa zote zinazohitajika ili kuwa mchezaji wa kiwango cha juu.
Kutokana na hali ya ukata wa kifedha inayopitia, klabu ya Barcelona inaweza kushawishika kumuuza kinda huyo iwapo watapata ofa nzuri.